GET /api/v0.1/hansard/entries/137999/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 137999,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/137999/?format=api",
    "text_counter": 447,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "maji ya Mzima Spring, ni heri kwanza watu wa eneo hilo wapate maji kabla ya kuenezwa maeneo mengine. Pili, Wakenya tumezoea kupoteza maji mengine sana. Mvua hunyesha lakini maji mengi hupotea. Ni lazima tuwe na njia mwafaka za kuweza kuhifadhi maji ya mvua hapa nchini. Sisi kama Wakenya tutafanya nini ili tuepukane na janga la njaa. Ingawa nchi ya Wayahudi ni jangwa, wao hukuza chakula kingi cha kujitosheleza na pia kuuza katika masoko ya nchi zingine. Sisi tuna nchi yenye rutuba na maji mengi lakini tunalia njaa. Ni jukumu letu kuhakikisha kuwa tutaweza kuyatumia maji yetu vizuri. Pesa ambazo zimetengewa Wizara hii hazitoshi. Serikali inatuhimiza kutotegemea kilimo cha mvua. Ni lazima tutegemee kilimo cha kunyunyizia maji mimea yetu. Je, pesa hizi zinatosha kufanya hivyo? Hilo ndilo swali ningependa Waziri na waheshimiwa Wabunge wezangu kuzingatia, ili tupige hatua za kimaendeleo pamoja. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}