GET /api/v0.1/hansard/entries/1380011/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1380011,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1380011/?format=api",
    "text_counter": 191,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika. Mimi ninajiunga na wenzangu kumpongeza Sen. Wakili Sigei kwa Taarifa aliyoleta kuhusiana na uhuru wa waandishi habari. Kidemokrasia, uhuru wa waandishi wa habari ni muhimu sana kwa sababu wao ndio wanaowajulisha wananchi na wahusika masuala muhimu yanayoibuka katika jamii. Imekuwa wazi sasa ya kwamba, magavana wengi na hata mawaziri wa Serikali kuu wanawanunua waandishi habari. Wale ambao hawawezi kununuliwa, wanatumiwa wahuni kuwapigwa, kutishwa na hata wengine wamewahi kupoteza maisha yao. Uhuru wa wanahabari ni kiungo muhimu cha demokrasia. Kama Seneti hatuwezi kuacha uhuru huo uhujumiwe na wale wanaoona ya kwamba ni bora kuficha yale matendo yanayofanywa kinyume na sheria ili wananchi wasije wakayaona. Kuhusu magavana, sasa wamepata moyo ya kwamba, wengi wakija hapa---"
}