GET /api/v0.1/hansard/entries/1380052/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1380052,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1380052/?format=api",
    "text_counter": 232,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "shirika la Telcom lilipata hasara na halijaweza kusambaza huduma nchini kote. Tukifungua ruhusa ya kupea kampuni zingine leseni za kusambaza umeme, watu wengi watapata umeme kwa urahisi. Madeni ambayo yamejaa katika shirika la KPC yanazuia shirika hili kupata faida. Kukosa faida inamaana kwamba hawataboresha huduma kwa wananchi. Mombasa kulikuwa na mtambo wa Kipevu I ambao ulikuwa unasimamiwa na Kenya Electricity Generating Company Plc (KenGen). Kipevu 1 ilikuwa kampuni ambayo ilikuwa inauza umeme kwa KPLC. Miaka mitatu iliyopita, Kipevu I ilifungwa. Mombasa tumebakia na Tsavo ambayo inaeneza umeme maeneo ya Mombasa. Ni kati ya mashirika ambayo yanaitwa IPPs. Gharama ya umeme kutoka mashirika haya iko juu kuliko ya KenGen. Hatuoni sababu ya KenGen kuzuiliwa kwani hii ni kampuni ya Serikali kama KPC. Kwa hivyo, ni rahisi mashirika haya kufanya biashara katika nchi yetu kuliko kutafuta wawekezaji wa nje kutengeneza umeme na kuuzia Kenya kwa bei ya juu. Hii ni njama ili Kipevu I ibakie vile bila kutumika halafu baadaye watu kwenye Serikali wauziane ili wauzie wananchi umeme kwa bei ya juu. Mwisho, umeme wetu mwingi unatokana na maji. Ina maana kwamba mvua isiponyesha kisawasawa inakuwa kwamba hakuna umeme wa kutosha. Pwani kuna ufuo wa bahari kutoka Lunga Lunga hadi Kiunga. Kwa kutumia mawimbi ya bahari, tunaweza kutengeneza umeme ambao utakuwa ni rahisi kuliko unaotumika sasa ambao unatengenezwa kutumia mafuta ya diese l, ambayo ni hatari kwa mazingira. Hii ni kwa sababu diesel ni mojawapo ya fossil fuels ambazo zinaleta mabadiliko ya tabianchi ulimwenguni."
}