GET /api/v0.1/hansard/entries/1380070/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1380070,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1380070/?format=api",
    "text_counter": 250,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Naibu wa Spika, muda ulipoendelea kusonga na kampuni hizo mbili zikagawanyika, kulikuwa na msukosuko kuwa kampuni ya KenGen itaanguka. Hata hivyo, walitia bidii na kufanya kazi jinsi ilivyohitajika na kuanza kuzalisha umeme kutumia mvuke. Hapo ndipo watu walianza kujua kuhusu uzalishaji wa umeme kutumia mvuke. Hiyo ilifanya kampuni nyingi kutaka kandarasi kwa kuwa ilisemekana kuwa KPLC ingekuwa inanunua umeme kutoka kwao kabla ya kusambaza katika sehemu za nchi. Wakati waliendelea hivyo, matapeli walianza kujiingiza na kuanza kusema jinsi wangesaidia KPLC kuzalisha umeme. Walipopewa nafasi, walianza kusajili kampuni nyingi. Watu hao walikuwa wafanyakazi wa KPLC. Kazi ya kampuni ya KenGen ilikuwa kuzalisha umeme. Wale wasiojua, mimi nilikuwa mfanyakazi wa KPLC. Baadaye nilihamishwa na kupelekwa katika kampuni ya KenGen. Nambari yangu ya kazi ilikuwa 348. Nilifanya kazi katika kampuni ya KenGen kwa muda wa miaka 30. Kampuni ya KenGen iliodhaniwa itaanguka iliendelea vizuri. Kampuni nyingi zilianza kuzalisha umeme baada ya kupewa kandarasi. Watu wa KPLC na KenGen walikuwa wanasambaza umeme kwanza pahali ambapo umeme ulikuwa unazalishwa kama vile Kiambeere, Masinga na Ishiara. Wakati huo, hata shule kama hii haikuwa na umeme. Ni aibu kubwa sana kwa KPC. Kuna sheria inayosema kuwa unafaa kuacha kitu kidogo pahali unafanyia kazi. Utapata kuwa hawajajenga hata shule au kufanya kitu chochote kwa sababu hawapati faida. Ilisemekana kuwa KPC ilianza kuwapa watu kandarasi za kununua transformers . Makosa yalianzia hapo. Walianza kununua transformers ambazo hazikuwa nzuri. Walinunua transformers nyingi zikawa zinatolewa kwa mlango wa nyuma. Transformers hizo pia hazikuwa zinadumu. Hilo lilikuwa tatizo la procurement . Kulianza kuwa na ukora katika KPC. Mara nyingi nyaya za umeme zinapitishwa kwenye barabara ya Serikali. Milingoti ya umeme ilipopita katika shamba la mtu, walikuwa wanafanya ukora ili pesa nyingi ilipwe. Ukora pia ulianza wakati wa kupitisha nyaya za umeme. Ilisemekana kuwa kukiwa na transformer karibu na shule, watu wangelipa shilingi elfu kumi na tano ili wasambaziwe umeme. Bei iliendelea kupanda hadi elfu thelathini. Ukora huo umekuwa ukiendelea katika kampuni ya KPC hadi leo. Ningependa kujulisha Seneti kuwa mwaka jana, nilileta Taarifa ambapo kufikia sasa sijapata majibu. Ilikuwa kuhusu umeme ulipopotea kwa muda wa masaa 24 na kusababisha vifo vya watu. Aidha, hali hiyo ilisababisha bidhaa za wafanyabiashara kuharibika. Hata hivyo, hakuna uchunguzi uliofanywa kuhusiana na suala hilo."
}