GET /api/v0.1/hansard/entries/1380072/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1380072,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1380072/?format=api",
    "text_counter": 252,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Katika miaka ya nyuma, kuna mambo mengi ambayo yalikuwa yakifanyika kama vile hesabu kutofanyika vizuri. Wakati mwananchi wa kawaida anaposhindwa kulipia umeme kwa muda wa miaka kama mitano, utakuta kuwa ana deni kubwa. Utapata kuwa kampuni ya KPC inadai watu pesa ambazo hawawezi kulipa. Bw. Naibu wa Spika, ningeomba kamati ifanye uchunguzi wa kutosha. Wanafaa kujua ugonjwa ulianzia wapi leo. Kuna madeni hadi leo. Ni vigumu sana kumpa mtu kazi na kukosa kumlipa. Madeni yote yanafaa kulipwa na mambo kulainishwa ili kampuni ya KPC iweze kufanya kazi jinsi inavyofaa. Serikali ya Kenya Kwanza imeahidi kuwa mambo mengi yatakuwa yanafanywa kwa njia ya haki. Kwa hivyo, Bw. Naibu wa Spika, mimi kama Seneta wa Kaunti ya Embu, naunga mkono Hoja hii. Nina huzuni mwingi kwa sababu Kaunti ya Embu ina sub-county nne. Kuna shule nyingi na watu wengi hawana umeme ilhali unazalishwa katika maeneo hayo. Nikimalizia, sehemu za kwanza kuzalisha umeme zilikuwa Masinga, Kamburu, Kiambeere na nyinginezo. Ilijulikana kama Seven Forks Dams. Mbili hazikukamilika. Kwa hivyo, kukawa na shida. Ni shida watu kulipa kampuni ya KPC kwa sababu hata kutoa mchanga ni shida. Ninapounga mkono, ningependa kusisitiza kuwa Ripoti hiyo iangaliwe vizuri. Asante, Bw. Naibu wa Spika."
}