GET /api/v0.1/hansard/entries/1380115/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1380115,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1380115/?format=api",
    "text_counter": 295,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Thang’wa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante sana Bw. Naibu Spika. Naomba kuchangia hii Ripoti kwa lugha ya Kiswahili. Hii ni kwa sababu kulikuwa na wanafunzi wa shule inayoitwa Kisima, nimeona ni vizuri niongee Kiswahili. Hapo jana, wakazi wa Kiambu walipokuwa wanaelekea nyumbani baada ya kazi, wengi wao walifika kwa nyumba zao wakapata giza. Walilala giza, wakaamkia giza na wameshinda giza mchana kutwa. Inasemekana kuna miti iliyoanguka karibu na nyaya za umeme kwa sababu ya mvua. Hivyo ni kusema kwamba, tukijadili Ripoti kama hii ambayo imetengenezwa na Kamati ya Kudumu ya Kawi, ni vizuri kukumbusha kampuni ya Kenya Power, iwe tayari tunapopata mambo ya dharura kama hayo. Nikichangia na kuunga mkono Ripoti hii, ningesema ya kwamba, Waziri wa Kawi, Mhe. Chirchir, akiwa na Katibu wa Kudumu wake, Mhe. Wachira, wanisikize. Wako na siku kumi na nne baada ya sisi kupitisha Ripoti hii kuleta ripoti ya waekezaji binafsi wa kuzalisha umeme. Wale Independent Private Partners (IPPs). Kenya mzima ingetaka kujua hawa watu ni akina nani na wametoka nchi gani wanaolipwa na Kenya kutumia dola ambayo iko juu sana. Tungetaka kujua hao ni akina nani. Sio hao tu, tungetaka kujua pia wenye hisa ambao wanamiliki hii kampuni. Ndio tujue ni wananchi kutoka nchi gani wanaomiliki Kampuni hii ya Kenya Power. Bw. Naibu Spika, Ripoti hii pia imeongea kuhusu ripoti ya ukaguzi wa fedha. Hiyo inamaanisha kwamba Mkaguzi wa Fedha anafaa kutuambia kiasi cha pesa ambazo zimetumika na kampuni ya Kenya Power kwa muda wa miaka mitano iliyopita. Tunafaa kujua pesa hizo huenda wapi wakati wananchi wa Kenya wanatozwa kodi wanaponunua umeme. Wengi hapa wamesema kwamba lazima tuondoe ukiritimba wa kampuni ya Kenya Power. Haifai kuwa na monopoly kwa sababu hiyo si kampuni pekee katika nchi nzima ambayo ina watu waliosoma na wanajua kuzalisha umeme. Eti lazima upate leseni kutoka kwa kampuni ya Kenya Power, ukitaka kuzalisha umeme kutumia jua. Tunafaa kumaliza monopoly ya kampuni ya Kenya Power. Naunga mkono yale yote yaliyosemwa na Maseneta. Bw. Naibu Spika, ningependa kumnukuu Rais wetu, Dkt. William Ruto. Wakati alipokuwa anatoa Hotuba yake ya kwanza katika Bunge. Alisema maneno ambayo yalilenga kumaliza monopoly ya kampuni ya Kenya Power. Alisema kuwa Serikali yake itakubali watu kujiunga katika vikundi. Vikundi hivyo vitapewa leseni za kuviruhusu kuzalisha umeme na kusambaza kwa nyumba za watu kule vijijini."
}