GET /api/v0.1/hansard/entries/1380117/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1380117,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1380117/?format=api",
"text_counter": 297,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Thang’wa",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Hiyo ni kumaanisha labda sisi ndio tumelalia masikio kama Seneti. Labda tungekuwa tumeleta Mswada hapa ili watu wa kule vijijini wapate fursa ya kuzalisha na kuuza umeme. Bw. Naibu Spika, kaunti zina jukumu la kuzoa taka. Katika nchi ambazo zimeendelea, taka ni rotuba. Unaweza kuzalisha umeme kutoka kwenye taka. Tunapeleka pesa nyingi kwenye kaunti ilhali hakuna kaunti yoyote katika nchi nzima ambayo imeanzisha mradi wa kuzalisha umeme ili kusaidia Serikali kuu kupunguza gharama za umeme ambazo zinaendelea kupanda. Endapo watazalisha umeme kutoka kwenye taka, itasaidia kupunguza gharama za umeme ambazo wanalipa kwenye hospitali na taa zinazowaka barabarani. Hakuna gavana yeyote amefanya hivyo. Hata kule Turkana, mahali ambapo jua linawaka mpaka usiku, hakuna mtu ameanzisha mradi wa kuzalisha umeme. Hii ndio maana tunaambia magavana kutumia pesa za umma vizuri wanapozipata. Hawafai kutumia pesa hizo kufurahisha au kuchekesha raia ama kupatia ‘vifaranga’. Bw. Naibu Spika, kule Kiambu, tunapewa mpaka samaki ambao wamewekwa kwenye vibuyu. Wananchi wengine wanawaweka kwa karai. Ni kama hawajui karai inatengenezwa kwa chuma. Inapopata moto, samaki wanakufa. Hivyo ni kusema kuwa ni vizuri wale magavana ambao tunawapa pesa wazitumie vilivyo sio kupatiana handouts. Nikimalizia, hili ni jambo ambalo Kamati ya Kawi inatakikana kuangalia; gharama ya umeme katika kaunti. Matumizi ya umeme yanalipwa na kaunti. Zikilipa, pesa inaenda kwa Kenya Power ambayo ni kampuni ya Serikali kuu. Inakuwaje Serikali kuu kupatia serikali za kaunti pesa kisha baadaye kaunti zilipe tena? Tunahitaji kufanya kitu. Bw. Naibu Spika, kama kaunti haina pesa za kulipia umeme, sio lazima Serikali kuu iwape ndio walipe. Jinsi wanavyosema, wanaweza kukata kwa kigingi. Badala ya kutuma pesa ndio walipwe, waikatie hapa kabla hawajapeleka kule, ili magavana ambao hawajui kufanya kazi wasije wakaumiza watu wetu. Wakishindwa kulipa gharama ya umeme za hospitali, wananchi wetu wanaumia. Ni vizuri pia tuangalie hilo ili umeme usije ukakatwa katika kaunti yoyote. Naunga mkono na nashukuru rafiki yangu, Seneta wa Kaunti ya Nyeri, ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Kawi katika Seneti. Wamefanya kazi nzuri sana. Ni vizuri tukipitisha Hoja hii, katika siku ambazo wamesema, 14 au 21, wale wote ambao wamepatiwa majukumu lazima wayatimize kwa haraka. Asante."
}