GET /api/v0.1/hansard/entries/1380981/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1380981,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1380981/?format=api",
"text_counter": 136,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": " Asante sana, Mheshimiwa Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ili nikaribishe wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mt. Kenya, Parklands Law Campus. Wamekuja na kiongozi wao, Bw. Swabir, ambaye ni mwanafunzi kutoka Lamu Mashariki. Watu wanasema watu wa eneo la Lamu Mashariki hawasomi. Hata hivyo, watu wamesoma, ingawa si wengi. Ninachukua nafasi hii niwaambie wanafunzi wa Lamu Mashariki kwamba watu wamekuwa wakisema anga ndio kikomo, lakini saa hii wanasema anga sio kikomo. Nafasi zipo. Wakitaka kusoma, wasome. Saa hii kuna bursary na wafadhili wengi. Kuna wafadhili wengi ambao husaidia wanaosoma sheria au udaktari. Vilevile, ninachukua nafasi hii niwakaribishe wanafunzi hawa na niwaambie nafasi hizi za Bunge ni zenu. Someni kwa bidii. Nyinyi ndio viongozi wa kesho na leo. Hamko mbali. Nyinyi pia mtakuwa katika Bunge hili wakati mmoja. Kila la heri. Nimefurahia sana. Karibuni sana katika Bunge hili. Asante."
}