GET /api/v0.1/hansard/entries/1381038/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1381038,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1381038/?format=api",
    "text_counter": 193,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Niweze kusema kuwa ijapokuwa nia ya kuleta Mswada huu ilikuwa nzuri, tukiangalia kwa undani, tunaona kuwa utawanyima wengine raha ya kufanya kazi kwa amani. Ninapinga marekebisho katika Mswada ambao umeletwa leo kutoka katika Bunge letu la Seneti. Wafanyikazi katika Taifa hili wameangaliwa vizuri na kuwekewa kanuni, sheria, masharti na mambo yao katika Katiba yetu. Katika kitengo cha ajira, wameangaliwa vizuri sana. Ukiangalia Mswada huu, mwajiri ndiye atalemewa sana. Katika Serikali yetu, tunataka mfanyikazi akiwa na furaha, mwajiri pia awe anafurahia akiangalia kazi yake. Hivi majuzi kule Mombasa, nilienda kuangalia sheria za wafanyikazi wa Export Processing Zone (EPZ) na tulielewana kuwa lazima haki za kimsingi za wafanyikazi ziangaliwe. Vile vile, haki ya mwajiri iangaliwe ili kukuwe na balance. Hii ni kwa sababu tunataka taifa ambalo linaweza kusonga mbele kwa mwafaka uliyowekwa katika Katiba."
}