GET /api/v0.1/hansard/entries/1381341/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1381341,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1381341/?format=api",
    "text_counter": 135,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante, Bw. Spika. Wafanyikazi wanaostaafu hukatwa pensheni kwenye mishahara yao wakati wana nguvu na wanapofanya kazi kwa bidi. Mwishowe, wakifika miaka ya kustaafu hawawezi kupata pesa zao. Swala hili limeleta hasara kubwa katika familia nyingi nchini. Kuna wazee ambao wamesomesha watoto wao, wanakuwa watu wazima ambao inatakiwa waende chuo kikuu na pia wajikimu kimaisha na kuishi maisha mazuri. Wanafanya kazi lakini hali ya pesa zao inakuwa kana kwamba ni wizi. Kwa mfano, ikiwa mfanyikazi aliweka pesa kwenye LAPTRUST ama LAPFUND, kaunti aliyoifanyia kazi inatakikana iweke pesa hizo kisawasawa. Mfanyikazi huyu anapostaafu, anakosa kupata pesa zake kutoka kwenye kampuni hizi. Mfanyikazi anakuwa hayuko kazini na hapati malipo ya kustaafu. Tukio kama hili linafanya wafanyikazi waliostaafu wakose pensheni. Wafanyikazi wengi wanapata taabu na kufa mapema kwa sababu hawawezi kufikia pesa zao. Wengi hufa na dhiki kwani pesa zao ziko ila hawawezi kuzifikia wanapougua. Hili ni kosa kubwa na lazima hatua ichukuliwe na mapendekezo ya Kamati kwenye hii Ripoti yatekelezwe. Nafikiria ingekuwa jambo nzuri sisi tukifuata yale mapendekezo yote ambayo hii Kamati ndugu yangu, Sen. Osotsi, ni Mwenyekiti. Wameandika hii pendekezo wakisema ya kwamba hii ndiyo taratibu ya njia tunaweza kuifuata na kuona ya kwamba wale waliokuwa wakifanya kazi na hivi sasa wako nyumbani, waweze kutumia hizo savings zao ambazo waliweka wakati walikuwa vijana. Cha muhimu ni kwamba, wale ambao hivi sasa wako katika majukumu haya na hususan wale magavana wako kwenye viti sasa, wahakikishe kwamba pesa hizi ambazo ni kama Ksh80 bilioni zinatumika vizuri. Pesa hizi ni nyingi. Watu waliostaafu wametapakaa kote nchini Kenya. Hivi sasa wanaishi katika maisha ya uchochole. Hii ni kwa sababu hizi pesa Ksh80 bilioni hazijapelekwa katika akaunti zao ili waweze kuzifikia na ziweze kuwasaidia. Bw. Spika, wengi wao hatuwezi kusema wanaishi siku zao za mwisho katika ulimwengu, lakini wamekaribia upande ule wa mwisho. Ingekuwa vyema kuona ya kwamba hatua mwafaka imechukuliwa na pesa zimepelekwa ili waweze kujikimu kimaisha. Ripoti hii imeandikwa vizuri na inapendekeza hatua ichukuliwe ili kuona ya kwamba waliostaafu wamepata malipo yao ya uzeeni. Sisi tunaona kama Bunge la Seneti litakuwa muhimu ikiwa hatua hiyo itachukuliwa mara moja ili serikali za kaunti ziweze kutuma pesa hizo kwa hazina ya kustaafu. Asante, Bw. Spika. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}