GET /api/v0.1/hansard/entries/1381363/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1381363,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1381363/?format=api",
    "text_counter": 157,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Ripoti ya Kamati ya Seneti inayohusiana na masuala ya uwekezaji na hazina maalum. Kwanza, naunga mkono Ripoti hii. Ni jambo la kusikitisha kwamba kaunti zetu zinadaiwa takriban Ksh80 bilioni. Hizo ni pesa za wale ambao wamestaafu na kwa sasa hawana mapato ya kila mwezi. Kaunti ya Mombasa ambayo nawakilisha inadaiwa Ksh9.43 bilioni. Jambo hili linaathiri kila mtu. Hata wale ambao wako kazini kwa sasa, uwezo wao wa kufanya kazi umeathirika kwa sababu mtu hajui akistaafu kama atapata malipo yake mapema au la. Niliwahi kufanya mkutano na County Public Service Board (CPSB) ya Mombasa. Tulipendekeza kuwa wale ambao wangestaafu karibuni, pesa zao zote zipelekwe kwa haraka ili wanapostaafu, kusiwe na malimbukizi ya pesa wanazodai, wanapostaafu, The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}