GET /api/v0.1/hansard/entries/1381368/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1381368,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1381368/?format=api",
    "text_counter": 162,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": ". Ni vyema mapendekezo haya yatekelezwe. Kama alivyosema Sen. Mungatana, kuundwa kwa kamati nyingine itakuwa kama kuzunguka mbuyu bila mwelekeo wowote. Hii ni kwa sababu wote ambao wametajwa katika Ripoti hii, kama vile Waziri wa Fedha na Mkuu wa Sheria, wako katika Intergovernmental Budget and Economic Council (IBEC). Kwa hivyo, wanajua kuwa pesa za pension hazipelekwi katika hifadhi ambazo zimewekwa na Serikali kusimamia pension. Itakuwa ni kama kupigia mbuzi gitaa wakati hakuna mwelekeo wowote. Naomba tukubaliane na Ripoti hii. Kupendekeza kuundwa kwa kamati nyingine ni kupoteza muda na vile vile raslimali muhimu ambazo zingetumika kushughulikia masuala mengine. Nikimalizia, kwa kuwa suala la pension ni muhimu, ijapokuwa wanatakiwa walipe riba kwa pesa ambazo hawakuzipeleka kwa wakati, riba pia haiwashtui. Ni vyema magavana wahusika wawe personally liable . Kama kuna gharama yoyote inayotakiwa kulipwa kwa sababu wamecheleweshwa kulipa pesa, basi iwe ya gavana binafsi kuliko riba kuongezeka kila siku. Ikiwa tumeshindwa kulipa kile kiwango cha chini, tutawezaje kulipa kukiwa na riba juu yake?"
}