GET /api/v0.1/hansard/entries/1381373/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1381373,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1381373/?format=api",
"text_counter": 167,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kavindu Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13733,
"legal_name": "Agnes Kavindu Muthama",
"slug": "agnes-kavindu-muthama"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii ili niunge mkono Mswada huu wa uhamishaji wa pensheni wa Kamati inayoongozwa na Sen. Osotsi. Ni aibu na haistahili, wala haifai kuwa magavana wanakata watu pesa zao za pensheni na kisha wakose kuzipeleka kule zinastahili ili wakati wafanyikazi wanastaafu, wapate malipo yao ya uzeeni. Mtu hufanya kazi ili wakati wa uzeeni, aweze kupata kitu cha kujisaidia. Wanapokatwa hizi hela, wanakuwa na matumaini makubwa ya kuwa, wakati wa uzeeni watakuwa sawa na salama. Bw. Spika, si hao wafanyikazi wa kaunti peke yao, pia kuna walimu. Hii ni kwa sababu ninaketi kwa Kamati ya Elimu na kuna walimu kutoka 2012 hawajalipwa pensheni. Hii inaumiza kwa sababu wengi wanakufa bila kupata hela zao. Ni lazima hii Kamati ione itachukua hatua gani zaidi ili kuhakikisha hizi pesa zimepatikana zote na zimehamishwa kwa hiyo hazina ya pensheni ili hao waliostaafu wafurahie pensheni yao kama watu wengine. Wakati wanapostaafu, wanapata shida nyingi sababu huo wakati hawana bima inayowaruhusu kuenda hospitali kutibiwa. Wakati huo ndio mgumu zaidi kwa sababu wengi huwa wanaugua magonjwa ya presha na kisukari na wanakuwa na shida nyingi. Bw. Spika, ninaunga mkono kwa kusema hatua ichukuliwe kwa hao magavana na kwa watu waliyo kwenye wizara zingine ambazo huwa hawapeleki hizo pesa za pensheni kwa ile hazina inayostahili. Asante. Naunga mkono."
}