GET /api/v0.1/hansard/entries/1381381/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1381381,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1381381/?format=api",
"text_counter": 175,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Asante sana, Mustahiki Spika, kwa kunipa nafasi kuchangia Hoja hii kuhusu shida zinazowakabili wale watu waliostaafu kupata pesa zao za uzeeni. Kirinyaga ni mojawapo ya eneo ambalo kuna watu kama hawa. Mimi binafsi nimehuzunika nikizika babangu mdogo kule Kirinyaga kwa sababu ya cancer - na akafa bila kulipwa malipo yake ya uzeeni kutoka mwaka wa 2012 hadi alipokufa. Alikuwa akifanya kazi katika hospitali ya Rufaa ya Kirinyaga. Ni mojawapo wa wengi walionifikia wakilalamika kutolipwa pesa zao za uzeeni. Harambee nyingi zinazofanyika siku hizi ni kwa sababu ya watu wasiolipwa pesa zao za uzeeni ilhali walijitolea mhanga katika kupeana huduma katika serikali za kaunti. Ni jambo la kuhuzunisha kwamba hadi leo tunapoongea, hawapewi kipaumbele kuhakikisha wamelipwa pesa zao. Wengi wa wale wanaoteseka saa hii ni wa umri uliosonga na umri inavyosonga ndivyo mwanadamu ana shida na magonjwa mengi bila uwezo wa kujifanyia kazi kwa sababu udhaifu na kukosa nguvu inaandamana na uzee. Kwa hivyo, nimeona kwamba Kirinyaga waliketi na County Pensions Fund (CPF) na wakakubaliana kwamba wataanza The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}