GET /api/v0.1/hansard/entries/1381382/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1381382,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1381382/?format=api",
"text_counter": 176,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "kulipa pesa zao za uzeeni ila mkataba bado haujatiwa saini ili kuhakikisha wale watu wamepata pesa zao. Nashukuru kwa bidii iliofanywa kule Kirinyaga ila naomba kwamba waendelee kwa kila kaunti kupatia kipaumbele mipango ya kulipa pesa ya wale watu waliofanya kazi katika Kaunti zetu. Mizigo ambayo wale wazee wanapata ni sisi kama viongozi tunaokabili pamoja na watoto wa wale tuliokuwa tunajivunia kwamba wanafanya kazi katika gatuzi zetu za Kenya. Mustahiki Spika, nashukuru Kamati inayoongozwa na Seneta wa Vihiga, Sen. Osotsi, kwa kazi nzuri na ngumu walioifanya na kuweka nakala na stakabadhi ambazo tunazitegemea siku ya leo kuchangia katika Hoja hii na masaa mengi ya kazi walioifanya. Wazee wanafurahi. Wengi hata nikiwa hapa naona wameandika jumbe kwamba wanafurahi na kazi inayofanywa na Seneti, haswa kuhakikisha wamepata haki zao kama wazee waliojitolea kuhudumia taifa lao. Mswahili husema, mghala muue na haki umpe. Kwa hivyo, haki iwafikie wale waliostaafu. Asante."
}