GET /api/v0.1/hansard/entries/1381390/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1381390,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1381390/?format=api",
    "text_counter": 184,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa nichangie Hoja ya Sen. Osotsi kuhusu malipo ya uzeeni na yale ya National Social Security Fund (NSSF) na fedha nyinginezo. Niko na huzuni sana kwa sababu ya kaunti zilizoachwa na madeni na wale magavana waliokuwepo. Wale watu tunaotetea hapa, sio wale wa kaunti pekee bali ni vitengo mbalimbali ikiwemo taasisi ya waalimu. Wafanyikazi wa kaunti wako na shida nyingi. Ikumbukwe walipoajiriwa walikuwa wachanga. Tunajua ya kwamba mfanyikazi yeyote anapoajiriwa, pesa anazopata huwa ni kidogo. Pia, anapoajiriwa, huwa anaingia kwa madeni ya benki na kwa shyloc k na pesa zingine zinazokatwa benki pamoja na malipo ya uzeeni. Ni aibu kubwa sana tunapoona mfanyikazi anapostaafu baada ya kufikisha miaka 60 na anaendelea kuwa na shida. Ifahamike kwamba kama sio hawa wafanyikazi wa kaunti, kaunti zetu hazingekuwa imara. Watu hawa ndio wanasimamia shughuli za maombolezi na za makanisa kule mashinani. Hivyo basi, hawa wafanyikazi wameshikilia serikali katika kona zote lakini wanapostaafu huwa na shida nyingi. Kwa mfano, Kaunti ya Embu kwa wakati huu imechagua Gavana ambaye ni mchapa kazi lakini alikuta madeni ya wanakandarasi yakiwa takriban Ksh2 bilioni. Kwa hifadhi ya serikali, alipata yamkini Ksh500 milioni. Anapopata pesa, anajaribu kupunguza mishahara ambapo kila mwezi analipa Ksh2.5 milioni. Japo anafanya hivyo, Seneti inashinikiza alipe madeni ya watu. Hivyo, basi, unakuta kaunti nyingi ziko na shida kama kaunti ya Embu. Ingewezekana, Kamati hii ingependekeza jinsi ya kulipa pending bills ndiposa zile kaunti zenye madeni ziweze kuyalipa kwa njia inayofaa ili wafanyikazi wa kaunti waache kuumia. Hivyo basi naunga mkono lakini kuna njia mwafaka ingeangaliwa ili hawa magavana wasiwe na shida ya watakavyosaidia. Utakuta, kwa mfano, Kaunti ya Embu kuna shida nyingi na ndio hizo shida tunajaribu kutatua hapa. Mpaka tuangalie ni njia gani hizo kaunti zitaweza kupata pesa ambazo zinaweza kulipa hayo madeni ndio wafanyikazi wanapostaafu waweze kupata malipo ya uzeeni kwa njia ya haraka. Kampuni niliyokuwa ninafanyia kazi, ya KenGen, unapostaafu huwezi maliza miezi miwili kabla hujapata pesa zako. Kwa hivyo, ningeomba zile kaunti hazina madeni ziweze kusaidia. Miezi mitano kabla ya mfanyikazi kustaafu, rekodi zake zitengenezwe vizuri ili turekebishe jinsi ya kujenga maisha yao wakati wameenda nyumbani. Tunajua ya kwamba hawana pesa zingine. Tumeona baadhi ya wafanyikazi wanapostaafu, wanaugua hata kuaga dunia. Kwa hivyo, ni lazima tuangalie njia mwafaka ile tutasaidia hawa watu wa kaunti vile watakavyokaa vizuri. Naunga mkono. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}