GET /api/v0.1/hansard/entries/1381405/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1381405,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1381405/?format=api",
"text_counter": 199,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Korir",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bwana Spika. Nimesimama pia kuchangia Ripoti ya Kamati ya kuwalipa wafanyikazi wetu malipo yao ya kustaafu. Hii ni changamoto kubwa kwa wafanyikazi wetu kwa sababu wanakosa pesa zao baada ya kustaafu ilhali wamejikaza na kutumia muda wao kuifanyia Serikali kazi. Wamejinyima na kuekeza pesa ili mwisho waitumie wanapozeeka. Hii ni changamoto ambalo gatuzi zetu zinapitia. Inachangiwa na Serikali kuu kwa sababu kuna pesa ambazo ilifaa kutuma kwa kaunti ili, itumike kulipa pension . Nashukuru Kamati hii kwa kazi nzuri ambayo wamefanya. Kama Bunge hili litatekeleza mapendekezo haya, basi, kaunti zitasaidika. Sina mengi ya kusema. Naiunga mkono Ripoti hii. Asante."
}