GET /api/v0.1/hansard/entries/138141/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 138141,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/138141/?format=api",
    "text_counter": 589,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Dr. Shaban",
    "speaker_title": "The Minister of State for Special Programmes",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii niweze kuzungumzia juu ya mazingira na haswa kumuunga mkono Waziri anayesimamia maswala haya ya mazingira. Mazingira mazuri ndio uti wa mgongo. Bila mazingira mazuri, hauwezi kupata hayo mambo mengine yote kama vile maswala ya maji na afya tunayoyazungumzia. Yote haya yanategemea mazingira mazuri. Jambo la kusikitisha ni kwamba hela ambayo Waziri amepewa afanyie kazi ni tone la maji kwenye bahari Hindi. Ninasema hivi kwa sababu matatizo ya mazingira ndio yametuweka katika hali tuliyo nayo hivi leo. Hatuna chakula kwa sababu tumeharibu mazingira yetu. Ningependa kumukumbusha Waziri na pia kumpongeza kwamba katika zile hela nyembamba alizopatiwa, ameweza kusafisha Mto Nairobi. Kumbe inawezekana! Tumekuwa tukisafiri kwenda nchi zingine na kila mahali tunaposafiri, watu wanatuambia kwamba unaweza kuchota maji mtoni na uyanywe bila wasi wasi. Hapa Kenya tumekuwa tukichafua mito yetu. Kwa hivyo nataka kumpongeza Waziri Michuki ambaye ni chapa kazi. Angepewa pesa za kutosha ili aweze kuhakikisha kuwa ametimiza kazi yake."
}