GET /api/v0.1/hansard/entries/138147/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 138147,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/138147/?format=api",
"text_counter": 595,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Tumekuwa wananchi ambao wanapenda kuharibu na kukatakata miti ovyo ovyo. Ni lazima sisi kama Serikali tufanye bidii ya kuhakikisha kuwa kuna sheria ya kuwa mti usikatwe bila sababu. Mtu asikae tu na kwenda kwa chifu na kuamua kuwa wanakata miti. Kuwe na sheria ya kukata miti. Mtu akikata miti ovyo ovyo ni lazima apelekwe kortini na atozwe faini ngumu ambayo itawaogopesha hata wale wengine wanaoharibu mazingira. Ni lazima tuwajibike kama Wakenya. Ni lazima tushikane na kusaidiana na Waziri wa Mazingira ili tuweze kufanya kazi pamoja na tuwe na makusudi ya kupanda miti. Serikali yetu inafaa kushikana na wananchi wetu na kulazimisha kupanda miti ambayo itaweza kurekebisha shida tulio nayo."
}