GET /api/v0.1/hansard/entries/1381524/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1381524,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1381524/?format=api",
"text_counter": 26,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa fursa hii ili niweze kuwakaribisha wandani wangu na rafiki zangu wa kisiasa na vilevile wapiga kura wangu wa Kaunti ya Bungoma. Seneti lina wanaume na wanawake wa tajriba na heshima kuu. Kule Kaunti ya Bungoma, unapowatazama, kuna mabinti ambao walipambana kisiasa kuwabwaga wanaume na wanawake kwa njia ya kidemokrasia. Bungoma ni Kaunti ambayo inajulikana kwa kutoa viongozi wanawake ambao wanajua kazi wanayopaswa kufanya na kwamba kura wanayopata sio kwa sababu ya urafiki wa mahaba ama wa kidini au wa kibiashara. Langu ni kuwakaribisha wanawake ninyi shupavu na wanaume wenzangu kwamba hapa ndimo Seneta wenu huchapa kazi. Hili ndilo Bunge ambalo tunawatia msasa magavana na serikali zao. Najua wamekuwa hapa kuelezwa jinsi ya kutia msasa na kubukua vitabu vya hesabu vya kaunti ili kila shilingi iwajibikiwe na ifanye kazi kwa mujibu wa sheria. Mimi Seneta wenu nawakaribisha. Jihisi mko nyumbani na wapenzi wa Seneti. Sisi ndio watetezi wa ugatuzi katika Kenya hii. Miswada yote inayohusu ugatuzi lazima tuwatetee. Yale masuala ya pesa zenu zile ambazo mnataka msimamie, tuko na ninyi sako kwa bako. Zile fedha mnazotaka za magari na mjivinjari kama viongozi wengine pia tuko na ninyi. Msikate tamaa. Tutetee ugatuzi, tufanye maendeleo na Wakenya watatukumbuka kwamba sisi ndio watetezi wa ugatuzi. Kwa niaba ya Seneti, nawakaribisha wote msikize na mjionee wenyewe jinsi mlinitunuku nafasi na nitawafanyia kazi hii kwa uadhilifu na upendo. Nawatakia kila la heri katika majukumu yenu ya kutetea watu wa Kaunti ya Bungoma na ugatuzi katika nchi ya Kenya."
}