GET /api/v0.1/hansard/entries/1381796/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1381796,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1381796/?format=api",
"text_counter": 298,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii ili nichangie huu Mswada wa County Boundaries Bill . Sio mara ya kwanza kwa huu Mswada kuja hapa. Ulikuwa katika Bunge lililopita lakini ulipata maafa katika Bunge la Kitaifa na haukupita ukawa sheria. Nianze na pale Mhe. Mungatana alipomalizia ya kwamba, tusidanganyane ya kwamba haiwezekani kubadilisha mipaka. Ibara ya 188 inasema kwamba inawezekana kubadilisha mipaka ya kaunti. Kwa hivyo, yeye kama mwanasheria na nafikiri wanasheria walihusika moja kwa moja kuandika Katiba, sioni vipi kipengele hiki kilijipata katika Katiba. Kinasema ya kwamba mipaka ya kaunti inaweza kubadilishwa. Naye anasema kwamba tusindanganyane, haiwezekani. Inawezekana. Huu Mswada ni muhimu sana kwa jimbo langu la Taita/Taveta. Hii ni kwa sababu, kama vile wasemaji wengine wamesema, tumepata changamoto za mipaka na kaunti tatu ikiwemo Kaunti ya Kwale, pale Mackinnon Road, Kaunti ya Makueni, pale Mtito Andei na Kaunti ya Kajiado, kule Rombo. Wale watu wa Taita-Taveta wanasikia wamefinyika. Hasa wale wazee ambao wanasema kwamba, wametuchagua kama viongozi lakini tunaacha mashamba yao yanachukuliwa. Hawajui watoto wetu watakuja kuishi wapi. Bw. Naibu Spika, kwa hivyo, namshukuru Sen. M. Kajwang’, Seneta wa Homa Bay, kwa kuuleta huu Mswada kwa hii Seneti tena. Hii ni kwa sababu ukipita, utapea uhai Ibara ya 188 ambayo inaangazia mambo ya kuangalia mipaka ya counties . Mipaka ya counties ambayo tunayajua kwa sasa iko katika sheria ya mikoa na wilaya ya mwaka wa 1992; Districts and Provinces Act 1992 . Vile mipaka ilivyo elezwa, imeelezwa ikitumia vipengee vya kimwili ama physical features ambazo ni barabara, The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services, Senate."
}