GET /api/v0.1/hansard/entries/1381797/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1381797,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1381797/?format=api",
    "text_counter": 299,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "mito na kadhalika. Na kama vile wasemaji wengine wamesema, hivi vipengee vya kimwili vinayoashiria mipaka vinabadilika. Mito inabadilisha mkondo, barabara ambazo zilikuwa zinatumika kuelezea mipaka, kwa mfano, barabara ya maaram iliyopita upande huu, kwa sasa, barabara za maaram zimekuwa nyingi na pia barabara nyingi zimekwa lami. Bw. Naibu wa Spika, ni vyema tuunge mkono huu Mswada uliyo katika mbele ya Bunge hili. Wakati huu Mswada utapelekwa katika Bunge la Kitaifa, tutumie njia zozote kusaidia ili upite na uwe sheria ili isaidia kulainisha hii mipaka yetu. Ukienda katika kaunti ya Taita-Taveta, maeneo kama Mackinnon Road, inasemekana kwamba Mackinnon Road iko ndani ya Kwale. Ukiangalia, walimu wa shule ya Mbele Sekondari, kwa mfano, wanatoka kaunti ya Taita Taveta na shule yenyewe imejengwa na Constituency Development Fund (CDF) ya Voi. Lakini inasemekana iko Mackinnon Road. Kwa hivyo, Mswada kama huu ukipita, utalainisha hizo tofauti ambazo ziko kule mashinani. Leo niangalia taarifa ya saa nane kwenye runinga na nikaona watu wa Kaunti ya Kajiado wakiandamana. Wanasema ya kwamba kuna shida ya mipaka. Pia sisi watu wa Taita-Taveta tumelalamika kwa sababu, magavana wa Kajiado na Taita-Taveta walishirikiana na wakapeana maelfu ya ekari za shamba iliyokuwa ya Taita-Taveta kwa watu wa Kaunti ya Kajiado. Huu Mswada unaangazia njia za kuhakikisha ya kwamba pale kuna utata wa mipaka, basi haya mambo yana sawazishwa. Shida za mipaka zimepelekea kudorora kwa usalama. Shida ya mipaka sio ya Taita-Taveta peke yake, kuna shida ya mipaka kati ya Meru na Isiolo, Kisumu na Kericho na Kadhalika. Hata, nimeona watu ambao wanaonekana kama ni watu wamoja, watu wa Kisii na Nyamira, watu ambao wanaongea lugha moja na wanaelewana wana shida ya mipaka. Kwa hivyo, kama kutasuluhishwa kudorora kwa usalama katika nchi yetu ya Kenya, ni vyema huu Mswada uungwe mkono na upite ili tuwe na sheria isulihishe haya masuala. Swala ambalo ni nyeti ni hii own source revenue . Kwa sasa hivi, kaunti zinahimizwa zikusanye ushuru. Ushuru mwingine ni huu wa own source revenue ambayo ni business permits, market charges na kadhalika. Kwa hivyo, kupigana kati ya kaunti mbili tofautitofauti inatokea kwa sababu kaunti zinaona ya kwamba zimeleta majengo na biashara zinaendelea, lakini hazitapata ushuru. Kwa hivyo, katika kutengeneza hii tume ya kuangalia mambo ya mipaka, mambo kadha wa kadha yamelainishwa. Ibara ya 188 haikueleza ni vipi hii tume itatengenezwa, lakini Mswada huu wa County Boundaries Bill, una maelezo moja kwa moja. Kwa mfano, qualifications za hao watu wa tume. Bw. Naibu wa Spika, mimi naunga mkono na ningependa kuambia wengine ambao watachangia huu Mswada wauunge mkono kwa sababu utasadia kaunti zetu kuendelea mbele. Kwa hayo machache, ninaunga mkono. Asante."
}