GET /api/v0.1/hansard/entries/1381900/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1381900,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1381900/?format=api",
    "text_counter": 70,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Sifuna",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13599,
        "legal_name": "Sifuna Edwin Watenya",
        "slug": "sifuna-edwin-watenya"
    },
    "content": "Kwanza nimjulishe Seneta wa Meru kwamba nimefanya kikao pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Usafiri, Sen. Thang’wa na yule ambaye ni Balozi wa nchi ya Japan kuhusu shida za trafiki katika barabara ya Ngong. Ametuahidi kwamba Serikali ya Japan kupitia ushirikiano na Serikali ya Kenya itazindua mfumo wa mabasi ya kasi katika barabara hiyo ya Ngong. Natumai itakupelekea kupata nafuu unapofika kazini hapa katika Seneti. Jambo la pili ni kwamba mimi ni baadhi ya wale wanaokaa katika Kamati ya Kuratibu Shughuli za Seneti. Kwa kweli tunapata msukumo kutoka kwa hao wenzetu ambao tunawakilisha katika Kamati ile. Ukiangalia ratiba ya Maswali ambayo yalikuwa yashughulikiwe leo, Mhe. Enoc Wambua ametoka Kitui leo asubuhi ili aweze kuuliza Maswali yake kwa yule Waziri wa Babarara na Usafiri. Kuna maswali mengi hata mimi nilikuwa nataka nimuulize Waziri wa Masuala ya Kifedha kuhusu mfumo mzima wa E-Citizen ambao Wakenya wengi wanatusukuma tufanye jambo juu yake. Kwa hivyo, ni jambo la kuvunja moyo sana, haswa kwa Waziri Aisha Jumwa ambaye nilimuona juzi akiwa maeneo ya kule Western akiwarai wakaazi wa Vihiga kutoruhusu viongozi fulani iwapo maoni yao yatakinzana na maoni yake ama maoni ya watu wa mrengo wake. Nilishtuka sana kwa sababu najua Mawaziri hawafai kujiingiza katika siasa. Na aliibua hisia kali sana kwangu kwa sababu alizungumzia suala ambalo lilikuwa linanihusu wakati mmoja nikiwa katika eneo bunge lake."
}