GET /api/v0.1/hansard/entries/1381925/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1381925,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1381925/?format=api",
    "text_counter": 95,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Sifuna",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13599,
        "legal_name": "Sifuna Edwin Watenya",
        "slug": "sifuna-edwin-watenya"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kuniokoa kutoka kwa mikono ya Seneta wa Meru. Kwa kweli mimi ni mwakilishi pale SBC wa hawa wenzangu hapa. Ni muhimu kwamba yote yanayoendelea pale tuwajuze kwa sababu kama vile umesema wewe mwenyewe, hakuna siri. Kwa hivyo, mimi naomba kuwe na mfumo hata kama arafa itaandikwa kwa yule Seneta aliyekuwa ameuliza mwenyewe pasina kuweka paruwanja kama vile ulivyosema. Mwenye kuuliza maswali haya ajulishwe kwamba kwa bahati mbaya ama kwa sababu moja ama nyingine, yule Waziri aliyekuwa anataka kumuuliza maswali hatafika ili watu waweze kujipanga. Ni vizuri tuwe hapa kwa ajili ya shughuli zingine za Seneti. Natumai kwamba kikao hakitatibuka kwa huu utovu wa nidhamu ulionyeshwa na wale Mawaziri kama Aisha Jumwa. Nakushukuru, Bw. Spika."
}