GET /api/v0.1/hansard/entries/1381952/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1381952,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1381952/?format=api",
"text_counter": 122,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kanuni ya Kudumu 51(d) ambayo Sen. (Dr.) Khalwale ameitaja ina adhabu kubwa sana kwa hao Mawaziri ambayo ni kuleta hoja ya kuwatoa kazini. Lakini, mimi ningefikiria ya kwamba SBC wangekaa ili tubadilishe ama tuiongezee sheria hii. Bali na kutumia nyundo kuua inzi, tungeweka kwamba ikuwe ni automatic. Waziri akikosa kufika kwa mara ya kwanza, bila kuuliza swali ni milioni moja. Mara ya pili iwe ni milioni tano na Waziri analipa yeye mwenyewe. Mara ya tatu, tuleta hoja kupitia Kanuni ya Kudumu 51(d). Ninaomba wenzetu ambao wanakaa kwa SBC, watengeneze kitu ambacho tunaweza kukitumia kiwe ni automatic. Sio lazima, Bw. Spika, awe akitoa ruling . Ukikosa kufika mara ya kwanza ni milioni moja, mara ya pili iwe ni milioni tano, mara ya tatu iwe ni hoja na iwe ni automatic, sio kitu ambacho tunakuja kudebate . Bw. Spika, tukigeuza Kanuni za Kudumu zetu, itatusaidia kupeleka message kwa hawa wenzetu ambao wamekaa kwa nafasi hizo, ya kwamba ni lazima tuheshimu Seneti na pia tuheshimu nafasi ambazo sisi tunafanya kwa niaba ya wananchi."
}