GET /api/v0.1/hansard/entries/1381966/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1381966,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1381966/?format=api",
    "text_counter": 136,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia. Mwanzo, nakashifu mazoea ya Mawaziri kukosa kuja kwenye vikao vya Seneti ilhali, kwenye orodha ya shughuli bungeni tulikuwa tumenukuu mambo kadhaa ili tuweze kuyaangazia. Naungana na Sen. Mungatana kupinga kutumia Kanuni za Kudumu nambari 51(d) kwani tutakuwa tumetumia nguvu nyingi kwa Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Ustawi wa Jamii. Wengi walioongea wamesema Waziri wa Barabara na yule wa Fedha walipeana sababu tosha, lakini waziri wa jinsia achukuliwe hatua kali. Kama vile Sen. Mungatana alivyopendekeza kwenye SBC, tuweke faini ambayo tutapiga Waziri kabla ya kumtimua. Faini ya shilingi milioni moja ama tano. Waziri akikosa kufika hapa kwenye Bunge hili tuangalie kama amepeana sababu ambayo inafaa. Pengine ameenda shughuli rasmi ambayo hawezi kukosa kwenda. Sen. Oketch Gicheru amesema kwamba yule Waziri ameenda mahali ambapo kunafaa. Sababu yuko mbele ya Kamati ya Fedha na Bajeti, na hangeweza kuja. Nakubaliana na Sen. Mungatana kwamba kuwe na mfululizo mzuri. Leo ni Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Ustawi wa Jamii anatuhumiwa kwa kutokuja. Kuna wakati ambao nilingoja Waziri wa Usalama, nikiwa nimejitayarisha na maswali kwa sababu wakaaji wa Laikipia walikuwa na changamoto na maswala ya usalama. Vilevile shida nyingi ambazo watu wanapitia Kaunti za Elgeyo Marakwet na Baringo. Tunapanga maswali ya kuuliza lakini Waziri anasema kuwa hataweza kuja. Sababu ya kutokuja inatosha kwani ataashiria kuwa kulikuwa na maafa Lamu. Haya ni mambo ya dharura. Nakubaliana na Sen. Mungatana mia kwa mia. Waziri anaweza kuwa na upendo na anataka kuja. Hata hivyo, tusije tukakejeliwa kama Seneti kwa kufanya jambo hili liwe mazoea. Kwa mfano, tukubaliane kuwa leo, Waziri Murkomen, asije. Kama mawaziri hawatakuja kuyajibu maswali hapa, basi tuondoe kwenye Kanuni zetu za Kudumu. Tukutane na wao kwenye mazishi na kuwauliza maswali ama kwenye kamati zetu kama desturi ya awali. Nakubaliana na wale walioongea awali ila namuuliza Sen. Oketch Gicheru na Mratibu wa walio Wengi, Sen. (Dr.) Khalwale, kuwa kwa leo tusilete hoja ya kumtimua Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Ustawi wa Jamii. Waziri aarifiwe kuwa amefanya makosa. Maseneta wengi wanakurai kuwa uandike barua ama utoe hukumu ikiwaelekeza wafike kwenye Bunge hili kwa dakika 30. Nakuomba kwa leo uarifu mawaziri hawa kuwa kosa limetendeka na kutoa msimamo mkali. Tusimame wima kama Bunge la Seneti ili tusidharauliwe na kukejeliwa. Nashtumu kitendo kilichotendeka. Asante kwa kunipa fursa hii."
}