GET /api/v0.1/hansard/entries/1381994/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1381994,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1381994/?format=api",
"text_counter": 164,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Mawaziri wote wameandika barua na kweli nakubaliana na Seneti kwamba, Waziri Aisha Jumwa, ameandika barua kwa kuchelewa. Hata hivyo, katika kauli za Maseneta wenzangu walipokuwa wamesimama kuzungumzia kutamaushwa kwao, hakuna hata mmoja ambaye amekupa wewe rai ya kuweza kumtafuta Waziri na kumuuliza ni kitu gani haswa ambacho kimemfanya yeye asiweze kufika hapa leo? Wameweza kuwaelewa Mawaziri wengine na wakakubali zile changamoto ambazo wamesema wako nazo. Kwa nini iwe ni Waziri Aisha Jumwa pekee yake na ni Mawaziri watatu ambao sote tumerauka ili kuja kuwauliza maswali? Masuala ya jinsia ni ya kila mtu, sio ya jinsia ya kike pekee yake. Kweli tulitamaushwa na yale yaliyoendelea katika ripoti ya NADCO, lakini ilibainika wazi ya kwamba viongozi wa kike tulikwenda kupitia majopo tofauti tofauti na tukatoa hisia zetu. Hata hivyo, wanakamati wa NADCO wenyewe waliamua kwamba watawachia majukumu hayo Wizara na ile Kamati ambayo alibuni ili waweze kupea mwelekeo sahihi ambayo wanataka. Waziri Aisha Jumwa, hakuna mkono wowote ama lengo lolote la kuweza kuondoa azma ya wanawake kufikia jinsia ya theluthi mbili katika Katiba yetu ya Kenya. Ningependa pia ---"
}