GET /api/v0.1/hansard/entries/1381998/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1381998,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1381998/?format=api",
    "text_counter": 168,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika kwa nafasi hii. Ni jambo la kutamausha sana sisi kama Maseneta kurauka asubuhi na mapema, wengine kupuuzilia mbali staftahi ili tuje tujadili mambo muhimu ya Serikali na nchi ya Kenya. Bw. Spika, baadhi ya Mawaziri ambao wamealikwa hapa ni lazima wajue kwamba kuja kwao hapa kutatoa mwelekeo na suluhisho ama kupea matumaini kwa Wakenya. Mhe. Rais amekuwa akizuru pembe mbalimbali za nchi ya Kenya akiahidi na kupea mwelekeo kwa miradi ya maendeleo kwa Wakenya. Miradi hii ambayo yeye hupea mwelekeo, wale ambao lazima watekeleze ni Mawaziri ambao wachache wao wamealikwa hapa na wamefeli kufika. Waziri wa Barabara na Uchukuzi anajua jinsi viongozi, kwa mfano, wa Mkoa wa Magaribi, hususan Bungoma, wamekuwa wakidai na kuitisha uwepo wake mashinani ili ajionee na aelewe ni sababu zipi zinashinikiza sisi kudai miradi ya maendeleo na barabara. Barabara ya Musikoma kwenda Mungatsi, barabara ya kutoka Kakamega kuja Musikoma na barabara kutoka Chwele kwenda Lwakhakha, ni lazima Waziri huyu aamke kutoka usingizi wa pono, atembee wima na ajue Kenya tunalipa ushuru. Hatutangoja Mhe. Rais azuru, atuahidi peupe mchana na Waziri amejifunga kwenye mahandaki akipora na kufurahia jasho la Wakenya. Juzi nimeuliza Maswali hapa kuhusiana na mimba za mapema."
}