GET /api/v0.1/hansard/entries/1382006/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1382006,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1382006/?format=api",
"text_counter": 176,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "kuimarisha biashara za akina mama na wajane. Waziri huyu mpaka leo ameweka nta kwenye maskio na kinywa chake amekifunga kabisa. Tunajiuliza haya maswali kwa sababu alichaguliwa kwa mrengo wa Kenya Kwanza. Ni lazima adhihirishe uwezo wake wa kuchapa kazi kwa kutembea katika pembe zote na kujadili masuala haya na wananchi wa Kenya. Bw. Spika, haya maswali, yeye na Waziri wa Elimu lazima watembee pamoja kusuluhisha masuala ya mimba za mapema na masuala ya wanawake na watoto katika taasisi za elimu katika nchi ya Kenya. Sasa kile tunasema sio kwamba tunaomba ati tafadhali waje, lazima waje. Mimi niko tayari kujiunga na Maseneta wengine, kwamba kila mtu lazima awajibike. Mtozwa ushuru anatoa jasho na kusaga meno kwa pesa anazotoa. Serikali inalazimisha watu walipe ushuru. Wale wanaochukua ushuru wanafurahi na kutupigia makofi kwa kulipa ushuru. Hata hivyo, tunapouliza uwajibikaji, wanatugeuka sisi na wanasema hatuwaheshimu na hatuwapi nafasi."
}