GET /api/v0.1/hansard/entries/1382008/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1382008,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1382008/?format=api",
    "text_counter": 178,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa ruhusa niweze kuchangia kuhusu Mawaziri ambao hawataki kufanya kazi kulingana na sheria tuliyopitisha. Nataka kuwakumbusha Mawaziri wote wakati tulikuwa tuking’ang’ana kuhusu vile watakuwa wakija katika kikao hiki. Ilikuwa ni vute nikuvute kati ya Serikali ya Kenya Kwanza na muungano wa Azimio. Lakini tulifaulu na ikakubalika kuwa tutakuwa tukiwaita kwa kikao hiki. Katika kikao hiki tunafaa kuwa kitu kimoja bila mgawanyiko. Waziri ametukosea, haswa mimi kama Seneta wa Kaunti ya Embu. Siku ya leo ni siku kubwa katika Kaunti ya Embu ambayo Gavana mchapakazi wa Kaunti ya Embu amejikakamua kwenda kwa kikao cha Embu County Assembly kuwaambia vile amefanya kazi kwa kipindi cha mwaka mmoja. Ni aibu kubwa sana ikiwa sijahudhuria pale kwa sababu katika kikao hicho, inafaa Gavana na Seneta wawepo, ili waeleze vile kazi imefanyika. Waziri wa Barabara na Uchukuzi amefanya mambo ambayo sio mazuri. Watu wa Kaunti ya Embu kutoka Makutano, Mwea, Embu, Tharaka-Nithi hadi Meru wanataka kujua barabara itapanuliwa namna gani iwe kama zile zingine. Kama kuna kaunti imetengwa ni Embu. Pili, watu wa Embu waliniambia nisikanyage pale mpaka nije hapa niulize Bw. Murkomen atatujengea lini uwanja wa ndege. Watu wa Embu wanafanya ukulima wa miraa lakini usafirishaji wake ndio shida kwa sababu ya ajali za barabarani. Wamesema tujengewe uwanja wa ndege ili tuweze kupeleka miraa yetu ng’ambo, ili tukuwe na pesa mkononi. Pia, walinituma niulizie vile barabara ya kutoka Karaba kwenda Makima hadi Machanga itatengenezwa kwa kuwekwa lami. Pia, vile barabara ya kutoka Kiritiri kwenda Karii hadi Kiambere mahali stima inatoka, itawekwa lami kuenda sehemu zingine. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services, Senate."
}