GET /api/v0.1/hansard/entries/1382011/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1382011,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1382011/?format=api",
    "text_counter": 181,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika, kama angekuja, hayo ni maswali ambayo nilitumwa na watu wa Embu niulize. Kwa vile hayuko, amekosea watu wa Embu. Kaunti ya Embu iko na Subcounty nne. Tungemuuliza haya maswali kwa sababu tunataka miaka inayokuja, Kaunti ya Embu iwe nzuri kimaendeleo. Waziri wa Fedha amekosea haswa kuhudhuria kikao hiki. Sisi katika Seneti ni wakubwa wake. Nilikuwa nimejiandaa kumuuliza kwa nini wafanyakazi wa Maseneta kama drivers na security hawajalipwa mishahara kwa muda wa miezi mitatu na huku amelipa wafanyakazi wa Bunge. Wafanyikazi katika ofisi zetu hawajalipwa kwa miezi mitatu na ofisi na Waziri wa Fedha. Nilitaka pia kumuuliza maswala ya waalimu wanaostaafu. Kwa muda mrefu walimu wamekuwa na shida. Sisi kama Maseneta tulifanya upelelezi tukaona ya kwamba mtu akistaafu akiwa miaka 60, anapata barua haraka lakini kupata pesa za kustaafu ndio shida. Hayo ndio maswali ningemuuliza. Naunga mkono vile hawa Mawaziri watachukuliwa hatua, lakini sio kuwatimua. Serikali ya Kenya Kwanza haisemi mambo ya kutimuana viongozi bali inatushauri kusemezana ili tuwafanyie kazi wananchi. Asante, Bw. Spika."
}