GET /api/v0.1/hansard/entries/1382381/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1382381,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1382381/?format=api",
    "text_counter": 267,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nakuru Town East, UDA",
    "speaker_title": "Hon. David Gikaria",
    "speaker": null,
    "content": ", kwa kunipatia nafasi hii ya kuchangia mjadala huu kuhusu madeni. Hakuna mtu, familia au nchi isiyo na deni. Huwa unakopa pesa ili ufanye nini? Kuna pesa zinazokopwa zisizo na faida yoyote nchini. Hata unapokopa pesa kwako nyumbani, lazima ujiulize utalipa vipi. Lazima uwe na mshahara wa kutosha. Kama ni Serikali inayokopa, lazima ikusanye pesa na iwe na mikakati ya kukusanya hela ambazo zitasaidia kulipa madeni hayo. Lazima ujiulize pia unakopa kutoka kwa nani? Ni nini kitakachofanyika ikiwa utashindwa kulipa? Tunapaswa tujiulize maswali mengi wakati tunakopa hela, iwe ni mtu binafsi au nchi. Wizara ya Fedha imetuelezea kuwa hatujatenda vizuri na tunajua hiyo ni kweli. Mhe. Spika wa Muda, unakumbuka kuwa pesa zilikuwa zinachukuliwa kufanya miradi ambayo haikuwa ya kuwekeza hela tu, ila ilitoa mapato pia. Hakuna wakati tuliambiwa kazi ambayo hela hizo zilifanya au njia zilizotumika ili tuseme kwa Kiingereza kuwa tumepata"
}