GET /api/v0.1/hansard/entries/1382385/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1382385,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1382385/?format=api",
"text_counter": 271,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nakuru Town East, UDA",
"speaker_title": "Hon. David Gikaria",
"speaker": null,
"content": "inataka kufanya, sana sana kuhusiana na haya maneno, lazima kipitie katika Jumba hili. Ikiwa Jumba hili litapitisha mambo hayo, hatuwezi kumlaumu mtu mwingine. Lawama ni kwetu sisi Wajumbe. Lazima tukae chini na tujiulize pesa tunazokopwa ni za kufanyia nini. Tutapata mapato gani tukikubalia Serikali ikope pesa ili ifanye miradi? Tutaweka mikakati gani ya kupunguza madeni? Tunaishukuru Kamati husika kwa kazi nzuri iliyofanya katika Ripoti hii. Tunaomba kuwa isiwe tu matamshi na kuandika maneno kwenye karatasi kisha turudi kufanya kinyume na ile mikakati tulioweka. Kuna njia nyingi ambazo ndugu zetu katika Wizara ya Fedha na Kamati ya Bajeti wamezingatia lakini ni muhimu tusipitishe madeni haya kwa watoto ambao bado hawajazaliwa. Tunapoyachukua haya madeni, ni lazima kila mtu abebe mzigo wake kwa wakati unaofaa. Ni makosa sana mimi nibebe mzigo na nimwachie mwingine aje alipe kama vile ilivyotendeka. Nitaubeba mzigo wangu kwa sababu najua nina miaka fulani ya uhai, na nikimaliza miaka yangu, atakayekuja kulipa sio shughuli yangu. Bunge hili lina jukumu la The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}