GET /api/v0.1/hansard/entries/1382410/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1382410,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1382410/?format=api",
"text_counter": 296,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taita Taveta County, UDA",
"speaker_title": "Hon. Haika Mizighi",
"speaker": null,
"content": " Ahsante, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi nichangie Hoja hii. Naunga mkono Ripoti ya Kamati ya Deni ya Umma na Ubinafsishaji. Kukopa na kukopeshana kupo. Lakini ni lazima tujue tunakopa fedha kwa malengo na mikakati gani ya kuhakikisha tunaboresha maisha ya wananchi. Tumeona pesa zimekopwa mara nyingi na zinafika nchini. Baadaye, tunapata manung’uniko kwamba hazikufanya ile kazi ama hazikwenda kwa walengwa. Wakati tunakopa zile pesa, ni vyema tuwe na mikakati dhabiti ya kuzifanyia kazi."
}