GET /api/v0.1/hansard/entries/1382541/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1382541,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1382541/?format=api",
    "text_counter": 37,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": null,
    "content": "maeneo ya Pwani. Tusisahau kwamba kiwanda kikubwa cha korosho kilikuweko kwa miaka mingi. Mambo yaliyofanywa na Serikali iliyopita, ni Mungu tu anayeweza kuwatolea hukumu kwa kuwadhulumu wale waliokuwa wakikimiliki kiwanda kile, ambao walikuwa ni wenyeji wa Pwani. Tuna kiwanda kidogo cha bixa ambacho kimefufuliwa katika hatamu ya Serikali hii ya Kenya Kwanza. Shirika la Agriculture and Food Authority (AFA) limechukua hilo jukumu, na limekuwa mashinani kuona ni vipi linaweza kufufua ukuzaji wa bixa, na hatimaye kutengeneza viwanda ili watu wapate ajira. Hili zao la pamba sasa hivi lina kiwanda Pwani, ambacho katika wiki mbili zinazokuja, Rais atakizindua. Ni jambo la kufurahisha kuona kuwa Wapwani wameanza kuletewa viegezo vya kutega uchumi. Ninachukua fursa hii kuhimiza wizara husika kuwa ni muhimu kiwanda cha pamba kinapowekwa pale, kifikirie zao hili litaweza kupatikana vipi kuanzia kwa ukulima wake. Sasa hivi, hatuna mashamba ya pamba. Wenyeji hawana uzoefu wa ukulima wa pamba. Huo ndio ukweli. Kama ni uzoefu wa Wapwani, tuna uzoefu wa ukulima wa nazi, korosho na bixa. Kwa hivyo, kiwanda hicho kitakapojengwa, nasihi wizara husika ione ni vipi itaweza kuleta malighafi na pembejeo za kuhakikisha kwamba wenyeji wanahusika na wananufaika wanapoanza ukulima wao. Kwa mfano, walete matingatinga na mbegu ziwe ni za ukulima wa kisasa. Wakati unafanya ukulima na unategemea hali ya hewa, mara nyingi ukulima huo huwa hauwezi kuenda mbele. Kule upande wa kwetu, wizara husika ina jukumu la kuelimisha wananchi. Tunajua kwamba pamba ni mali, ni zao lililo na faida, na linaleta ajira. Hata hivyo, pia, elimu kuihusu ni muhimu. Wizara ikiweka kiwanda bila ya kuelimisha watu juu ya manufaa wanayoweza kupata na kufanya ukulima wao uwe mwepesi, kuna uwezakano wa kiwanda hicho kufanya kazi kwa kutumia malighafi kutoja sehemu zinginezo, ilhali hilo si lengo la Serikali. Lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wote, kuanzia pale chini, wananufaika na miradi yake yote. Ninampa kongole Mhe. Emaase, aliyeleta Mswada huu, na ninauunga mkono, kwani ni miongoni mwa zile ajenda za kutoa ajira, kuleta mali kwa Serikali, na kuhakikisha kwamba sarafu yetu inazidi kupata nguvu kupitia upunguzaji wa gharama za vitu tunavyopata kutoka nje ya nchi. Asante."
}