GET /api/v0.1/hansard/entries/1382876/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1382876,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1382876/?format=api",
    "text_counter": 130,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunifa fursa hii kuchangia Ripoti ya Kamati ya Fedha na Bajeti ya Seneti kuhusu Taarifa ya Sera ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2024/2025. Kabla sijachangia, Bw. Spika, najiunga nawe pamoja na Sen. Sifuna kuwakaribisha wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi. Nilikuwa mwanafunzi katika chuo hicho miaka 34 iliyopita. Kwa hivyo, hata nami najivunia kuwa mmoja wa waliosoma katika chuo hicho. Ripoti hii ni muhimu sana kwa sababu inatoa mwongozo wa Serikali kuhusiana na masuala ya bajeti ya mwaka utakaoanza Julai mwaka huu na kuisha Juni mwaka ujao. Napongeza wanakamati kwa kuchambua sera hii na kuona kwamba mambo kadha wa kadha yanayoathiri zaidi kaunti zetu yameangaziwa hapa. Bw. Spika, kumekuwa na malimbikizi ya pending bills; yani madeni yanayodaiwa Serikali kuu na serikali za kaunti. Madeni haya yanaathiri sana wawekezaji wa kibinafsi ambao wanafanya biashara na kaunti zetu na Serikali kuu. Ikiwa Serikali kuu na kaunti zetu hazilipi kwa wakati, ina maana kwamba wawekezaji wale wataingia kwa madeni na kupoteza rasilmali zao na mtaji ambao ni muhimu kwa kuendesha uchumi wa nchi hii. Jambo la pili ni kuwa kuna suala la kuajiri wafanyikazi wa afya 20,000. Tunajua kwamba afya ni mojawapo ya huduma ambazo zimegatuliwa. Kwa nini Serikali inaajiri wafanyikazi 20,000 wakati kila kaunti ina nafasi ya kuajiri watu hawa ilhali pesa zinazobaki kwa Serikali kuu ambazo zingepaswa kupungua katika kaunti zetu hazipungui? Bw. Spika, jambo la tatu ni kwamba Serikali ilikuwa imependekeza shilingi bilioni 391 ziende kwa kaunti zetu. Hiyo ingekuwa asilimia ndogo sana ya pesa ambazo zitapelekwa katika kaunti zetu. Gharama za huduma zinazotolewa katika kaunti zetu zimepanda. Mishahara peke yake imeongezeka kwa sababu kodi kadhaa ambazo zimeathiri mishahara zimeongezeka. Ukizingatia shilingi bilioni 385.425, ongezeko la mwaka jana lilikuwa asilimia 1.5. Kwa hivyo, nakubaliana na Kamati hiyo kwamba fedha ziongezwe kufikia shilingi bilioni 415. Bw. Spika, suala lingine ambalo ningependa kuchangia ni kuhusu contribution in"
}