GET /api/v0.1/hansard/entries/1382939/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1382939,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1382939/?format=api",
    "text_counter": 193,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa ya kuchangia Hoja hii. Ninaunga mkono Kamati ya Fedha na Bajeti katika Seneti kwa kazi nzuri waliyofanya ya kuangazia kazi ambayo kaunti zote 47 zitakuwa zinafanya. Ni vizuri kwa sababu mwaka uliopita pesa ambazo walipatiwa hazikutumika kufanya kazi kule mashinani. Pia naunga mkono kwa sababu pesa ambazo imeongezewa na zikawa shilingi bilioni415. Hata hivyo, pesa hizi hazitoshi. Wangeongeza shilingi bilioni 50 ili zifike shilingi bilioni 465 kama walivyoagizia magavana mwaka jana. Kama Maseneta, kazi yetu ni kupigania devolution kama vile magavana wanavyohitaji ili wafanye kazi. Wabunge wa Bunge la Taifa hawaonyeshi kazi wanayofanya kutumia pesa wanazopewa na Serikali. Kazi yao ni kupigana na kuteta kuhusu utendakazi wa magavana. Mwaka jana, pesa ambazo Kaunti ya Embu ilipewa hazikutosha kwa sababu ya"
}