GET /api/v0.1/hansard/entries/1382941/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1382941,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1382941/?format=api",
"text_counter": 195,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Gavana wa Embu ni Mhe. Cecily Mbarire. Kuna wage bill kubwa na kila mwezi analipa shilingi milioni 250. Kwa muda wa miezi minne, anatumia shilingi bilioni moja kulipa mishahara. Kaunti inabakia na kama shilingi bilioni moja na pending bills ni shilingi bilioni 2.2 bilioni. Vile vile, kaunti ilikuwa na deni la milioni 500. Gavana ameng’ang’ana na kulipa shilingi milioni 600. Baada ya miezi minne, alikuwa amebakisha kama shilingi 400. Pia kuna kazi zingine za ofisi zinazohitaji pesa. Raia wa Embu Kaunti wanateta kuwa hakuna kazi ambayo gavana amefanya. Hii ni kwa sababu asilima 30 ya pesa ambazo Seneti inampa inafaa zitumike kwa maendeleo. Magavana wengi wanajaribu kufanya kazi lakini haionekani. Naunga mkono kuwa magavana waongezewe pesa. Ni muhimu sisi Maseneta kuungana na kwenda kwenye kaunti tofauti ili kuona vile kazi inafanywa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services, Senate."
}