GET /api/v0.1/hansard/entries/1382942/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1382942,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1382942/?format=api",
    "text_counter": 196,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Mimi ni Naibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Kilimo ni kazi ya kaunti. Hata hivyo, pesa ambazo zinatengewa sekta ya kilimo zimepunguzwa. Wakulima wanafaa wasaidiwe ili kuuza mazao yao kwa bei nafuu na vile vile wawe na maji kwenye mashamba yao. Katika Hoja hii, hakuna pendekezo la kuongeza pesa za watu ambao wanafunza wakulima kuhusu kilimo bora. Kama Seneta wa Kaunti ya Embu, naunga mkono Hoja hii lakini pending bills na wage bill za kaunti hiyo zinafaa kuangaliwa. Kuna kaunti ambazo zimepewa pesa lakini hakuna kazi wanayofanya. Naunga mkono Hoja hii kwamba kaunti zipewe shilingi bilioni 415. Asante, Bw. Naibu wa Spika."
}