GET /api/v0.1/hansard/entries/1382981/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1382981,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1382981/?format=api",
    "text_counter": 235,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii. Mchango ni kwamba matarajio ya Wakenya yataweza kuafikiwa kutokana na pesa ambazo tunagatua kwenda mashinani. Juzi, magavana walidai kwamba pesa zimechelewa na miradi mingi ya maendeleo haijatimilika Wengine wamekuwa wakikenua vichwa wakidai tumepunguza mgao wao. Leo, mbele ya Wakenya wote, wamejionea wazi msimamo wa Bunge la Seneti. Tunataka waongezewe pesa ili ziambatane na majukumu yaliyogatuliwa katika Katiba Zile pesa ambazo kaunti zinawatozwa watu ni kama sadaka au kafara kule mashinani. Naomba hili Bunge la Seneti lifuate hizi pesa ili tuhakikishe zote zinazotozwa watu wa kaunti zetu, zinaweza kuhesabika na kuajibikiwa kwa miradi ya maendeleo. Ukipiga kurunzi mashinani, utagundua kwamba, baadhi wanaochukua ushuru mashinani ni matajiri kuliko Viongozi wa Wadi na Wabunge katika Kenya hii. Ndio kwa sababu tunataka mfumo mpya wa kuchukua ushuru kutoka kwa Wakenya. Haiwezekani wale wanaotoza ushuru waache kutumia mfumo wa kidijitali waanze kutembea na mikoba, wakichukua pesa kutoka kwa Wakenya na ukiuliza hesabu, wanasema uchumi ni mbaya. Bw. Naibu Spika, ugatuzi unawapa watu wa kaunti hizi kuimarisha shule za chekechea, shule za anuwai, ukulima, uchumi samawati na mazingira na miradi ya michezo. Ni lazima magavana wajue kwamba hizi pesa ni za kuhakikisha majukumu haya ya yanatekelezwa. Wakituona mashinani, watukumbatie na wafungue vitabu vya hesabu ili tuvikague na tuelezee watu wa kaunti zetu, pesa zetu zinatumika vipi. Yule atapatikana akipora pesa hizi, akubali kubeba msalaba wake. Ninashukuru na kuunga mkono mapendekezo ya Kamati ya Uchumi na Bajeti katika Seneti. Pia naomba Maseneta wote wapitishe ili tuanze kupambana na ufisadi kule mashinani."
}