GET /api/v0.1/hansard/entries/1383194/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1383194,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1383194/?format=api",
    "text_counter": 26,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Gilgil, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Martha Wangari",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika. Ningependa kuchukua nafasi hii kukuunga mkono na kuwakaribisha wenzetu kutoka Bunge Jirani la Tanzania katika Bunge la Kitaifa la Kenya. Ninaona wako sawa kwa sababu kuna akina mama na baba. Wamehakikisha ya kwamba kila jinsia imewakilishwa kwenye Kamati hiyo. Naomba tuendelee na demokrasia ya Bunge ili tulete uwiano mwema kwa jamii yetu ya Afrika Mashariki. Naomba tufanye kazi pamoja kama viongozi ili tulete uwiano na utangamano. Nawakaribisha nchini, na mtakaporudi Tanzania, muyaseme mazuri ya nchi yetu. Ni muhimu pia wajue ya kwamba Nairobi pekee ndilo jiji ambalo lina mbuga la wanyama. Nawaomba mtembee Nairobi na mkirudi kwenu, mpeleke salamu za Wabunge na za nchi nzima. Karibuni tena."
}