GET /api/v0.1/hansard/entries/1383909/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1383909,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1383909/?format=api",
    "text_counter": 741,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taita Taveta County, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Haika Mizighi",
    "speaker": null,
    "content": "Ahsante sana kwa kunipatia fursa hii. Naunga mkono Ripoti hii. Pia naipongeza Kamati ya Bajeti na Uidhinishaji wa Matumizi kwa kuiandaa na kuingalia kwa ufasaha. Kuna mengi ya kusifia katika Ripoti hii lakini, kwa sababu mengi yamesemwa, ningependa kuangazia pesa zilizotengewa uwakilishi wa akina mama. Pesa za NG-CDF zimeongezeka lakini zile za NGAAF hazijaongezeka na bado ni kidogo sana. Hata kama tunaunga Ripoti hii mkono, tunaomba Kamati hii itilie maanani maswala ya akina mama. Sisi pia ni Wabunge na tunastahili kuongezwa fedha kwa sababu tunashughulikia makundi mengi miongoni mwao wakiwa wazee, vijana na watu walio na mahitaji mbali mbali. Saa hivi, Wawakilishi wa Wanawake Bungeni wanapata Ksh9 milioni peke yake katika kila kaunti. Unapolinganisha fedha hizi na NGCD, inakuwa ni mzaha tu."
}