GET /api/v0.1/hansard/entries/1383944/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1383944,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1383944/?format=api",
"text_counter": 776,
"type": "speech",
"speaker_name": "Wundanyi, WDM",
"speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
"speaker": null,
"content": " Asante kwa nafasi hii. Kwanza, nachukua nafasi hii kumpongeza Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti kwa mambo makubwa ambayo amefanya. Amefanya kazi nzuri ndani ya wiki mbili na tuko na Ripoti tunayozungumuzia. Nataka kuongea juu ya mambo matatu kwa haraka, kwa sababu ya saa. La kwanza ni kuunga mkono Ripoti hii kwa sababu imeangazia maswala muhimu katika nchi yetu ya Kenya. Zote ambao tunaishi ndani ya Kenya tuna haki kupata mafanikio ya maendeleo katika kila sehemu ya Kenya. Katika nchi hii yetu, kuna maeneo mengi ambayo yamefaidika zaidi kutokana na mfumo wa Serikali uliokuwepo kutoka wakati wa uhuru mpaka sasa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}