GET /api/v0.1/hansard/entries/1383994/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1383994,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1383994/?format=api",
    "text_counter": 826,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Mswada huu ni wa maana sana. Tumeusubiri kwa miaka mingi. Ijapokuwa Mswada huu una mapengo kiasi, tusikose mwana na maji ya mtoto. Kwa hivyo, tuzungumze kuhusu Mswada huu, tuupige msasa na tupendekeze marekebisho wakati ufaao. Nasema hivyo kwa sababu, wakati Kamati ya mambo ya mazingira ilipozungumzia Mswada huu, ilisema ya kwamba tuukatae na tusiupitishe kama Bunge kwa sababu ya changamoto nyingi ambazo zilipatikana ndani ya Mswada huu. Chochote kizuri hakikosi ila. Sisi kama Bunge, tuna nafasi ya kuzizungumzia ila zilizoko katika Mswada huu na kuzirekebisha. Taifa letu la Kenya limebarikiwa sana. Lina mali asili tofauti tofauti kama maji, maziwa, mito, misitu, wanyama pori na bahari. Wakati mwingi, jamii ambazo mali asili hupatikana kwao hukosa mapato au kile ambacho hupatikana kutokana na mali asili. Vilevile, Serikali na kaunti zetu hukosa mapato. Mswada huu unazungumzia njia ambayo itatumika kufanya ugavi wa mapato hayo katika Serikali kuu, serikali za kaunti na jamii ambazo mali asili hupatikana sehemu zao. Ugavi huo utakuwa wa asilimia 60 kwa 40. Asilimia 40 itaenda kwa kaunti. Jee, hizi kaunti zitagawanya vipi asilimia hii? Kwa mfano, ikiwa jamii ya mali asili inatoka katika kaunti ya Mombasa na mali yake asili inatoka katika c onstituency ya Likoni, tukisema asilimia 40 itaenda kwa kaunti, itagawanywa aje? Kaunti inaweza kufanya miradi kutokana na asilimia hiyo katika sehemu zingine na isahau kufanya mradi katika ile sehumu ambayo mali asili ilipatikana. Katika kutengeza Kamati ambayo itaangalia ugavi huo utafanyika kwa njia gani, mwakilishi wa Mbunge hakuwekwa. Waliweka mwakilishi kutoka katika Baraza la Magavana pamoja na wawakilishi wengine. Inafaa tujue ya kwamba ugatuzi unaanzia eneo bunge. Kwa mfano, Kwale, kulikuwa na madini yanayoitwa: “Base Titanium.” Katika kuhakikisha kwamba jamii inafaidika, palitengezwa kamati ambayo ilikuwa na wawakilishi wa kutoka kwa kaunti, Serikali, Bunge na kwa wajumbe wa wadi zetu. Hivyo basi, sauti za wananchi wa chini ziliskika katika swala hili la mapato ya madini. Vilevile, wakati ugavi wa mapato unafanyika, lazima ujulikane. Kwa mfano, Base"
}