GET /api/v0.1/hansard/entries/1383996/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1383996,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1383996/?format=api",
    "text_counter": 828,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": "kule Kwale imepata mapato makubwa sana. Lakini je, yale waliorejesha kwa Serikali kuu, kaunti na jamii ni sawa na mapato yale? Mapato ambayo Serikali kuu, kaunti na jamii walipata ni duni sana. Mswada huu ungeangalia usawa wa mapato yanayopatikana katika biashara ya mali asili ili yafaidi Serikali kuu, kaunti na jamii. Vilevile, nataka nizungumzie swala la mazingira. Wakati mali asili imepatikana katika sehemu fulani na biashara inaendelea, kuna athari kwa mazingira. Je, Mswada huu umezungumzia athari hizo kinaga ubaga? Je, aina gani ya fidia itapatikana ili kuhakikisha kwamba mazingira yanaregeshwa katika hali yaliokuwa na yaendelee kuzalisha?"
}