GET /api/v0.1/hansard/entries/1383998/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1383998,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1383998/?format=api",
    "text_counter": 830,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": "wanaondoka kule Kwale, lakini ardhi ile ya ekari nyingi itabaki ikiwa haiwezi kutumika katika ukulima na ufugaji. Je, hasara kama ile itaenda kwa nani? Kwa Mkenya na Serikali kuu ya Kenya? Lazima tuangalie mambo haya. Commission on RevenueAllocation (CRA) ama Tume ya ugavi wa fedha itasimamia mikataba ya wale wanaotaka kutumia mali asili. Serikali kuu, wakaazi na kaunti wamepewa majukumu mengi sana kama kusikiliza malalamiko na kuhakikisha malipo yanafika kwa njia inayotakikana. Lakini hatujaonyeshwa kabisa mfumo maalum ambao utakuwa unafuatiliwa kuhakikisha kwamba mambo na majukumu hayo yamefanyika pasipo watu kutumia rushwa na njia ambazo zitawaathiri wale wanaohitaji kupata mapato yale. Pia, swala la mali asili kuweza kusaidia, tungependa kujua asilimia inayoenda kwa jamii. Je, fedha hizo zitatumika kwa njia gani? Je, kutakuwa na public participation ili watu waweze kuelewa haraka. Kitengo hicho hakijawekwa kuonyesha kama watu watakuwa na usemi katika miradi itakayofanyika kupitia mapato ya asilimia 40. Pengine kaunti inaweza kuamua kutumia ile asilimia 40 kufanya kitu bila kuhusisha walengwa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}