GET /api/v0.1/hansard/entries/1383999/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1383999,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1383999/?format=api",
"text_counter": 831,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": "Hizo ndio changamoto tumeona katika Mswada huu, ambao tumeupenda sana. Hii ni kwa sababu tunajua unaweza kujenga ajira na kuboresha uchumi katika Taifa letu. Lazima tuweze kuangalia yale mapato yanaopatikana kutoka kwa mali asili yetu. Zile fedha ambazo tunazungumzia za Serikali - ile asilimia 60 - tumeambiwa zitatengenezewa hazina fulani ya kuzisimamia. Kuzungumza kinaga ubaga, hazina hizo zitasimamiwa na akina nani? Watakaosimamia watakuwa watu wa tajriba gani? Zitakaa kwa muda gani? Kitengo gani kitaangalia mambo ya mazingira? Kitengo gani kitaangalia mambo ya jamii na kusaidia miradi ya kitaifa? Hatutaki kupitisha jambo bila kulipiga msasa. Huko mbele iwe fedha ziko pale, lakini pengine watu wachache wanazitumia kiholela au kutumia rushwa na kufanya pesa zile zisiweze kumsaidia Mkenya, ama yule haswa atakaye athirika. Ikiwa kaunti zimepakana, hatukuelezwa jinsi jopo litachaguliwa ili kusimamia na kuangalia hesabu ya mapato. Je, ni watu wangapi watakuwa katika jopo lile? Limesema tu ni kaunti, na kama ni kaunti tatu, je watachagua watu wangapi? Hesabu ile itageuka ama itakuwa vipi? Kuna mapengo kadhaa katika Mswada huu. Lakini huu ni wakati mwafaka. Kule Mombasa Pwani, mambo mengi yanafanyika pale bandarini. Je, wakaazi ama jamii watapata nini? Ingawaje hii haizungumzii madini. Lakini kule Taita Taveta kuna madini, Turkana kuna mafuta. Kuna mambo ya jua ambayo yanapatikana hata kule Lamu, ambako kulikuwa kufanyike mradi wa jua, lakini kukawa na changamoto. Hii ni kwa sababu, hatukuwa na sheria inayoweza kufuatilia mambo kama hayo. Sheria hii ikipigwa msasa, lazima ifwatiliwe kisawa ili isiweze kupingana na sheria zilizoko. Sasa hivi, tuna sheria inayoitwa Mining Act kwa lugha ya Kingereza na pia kuna sheria nyingi zinazozungumzia mali asili. Lazima pia tuweke ya kwamba hawatakua…"
}