GET /api/v0.1/hansard/entries/1385316/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1385316,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1385316/?format=api",
"text_counter": 396,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Olekina",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 407,
"legal_name": "Ledama Olekina",
"slug": "ledama-olekina"
},
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii kukaribisha wageni waliokuja katika Seneti kupeana maombi yao kuhusu hali inayoathiri usalama na kuyahatarisha maisha ya watu wa Samburu, Turkana, West Pokot na Baringo. Ni jambo la kusikitisha sana katika karne hii kuona kwamba watu bado wanapigana na kuuana. Hilo ni jambo la kuhuzunisha na kukera. Lazima sisi sote kama viongozi tusimame ili tuwasaidie wenzetu. Wamaasai wanaoishi kule Samburu wanaumia sana. Kila siku wanazika watoto wao waliokuwa wakiendelea na kazi zao. Nawaomba wanachama wa Kamati ya Usalama wa Taifa, Ulinzi na Masuala ya Kigeni watilie maanani maombi haya yaliyoletwa na wenzetu kutoka Samburu ili tuhakikishe kwamba wanaishi kwa amani. Ni aibu sana. Nimeona mama mmoja na wazee waliojikokota kutoka Samburu hadi hapa kuja kutulilia. Hiyo inamaanisha kwamba Wakenya wana imani nasi. Itakuwa vibaya sana watu hawa watoke kule Samburu hadi hapa kisha kilio chao kiambulie patupu. Tuliwaambia wakae hapa na kuona kwamba sisi pia tumekerwa na jambo hilo linalowakera na kwamba tutasimama nao. Hii ni kama nyuma yao na kilio chao ni chetu. Asante."
}