GET /api/v0.1/hansard/entries/1385326/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1385326,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1385326/?format=api",
    "text_counter": 406,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante, Bi Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa, nampongeza Seneta wa Samburu kwa kuchukua jukumu na kufuatilia mambo ya usalama katika sehemu ya Samburu. Usalama umekosekana sio Samburu peke yake, bali pia Laikipia na Baringo. Tunaisha kwa hali ya sitofahamu. Kwa hivyo, namshukuru hasa Seneta wa Nandi kwa sababu ameleta Mswada unaosema kwamba wizi wa mifugo wa kimabavu uwe ugaidi. Kwa hivyo, kazi kuu ya Serikali ni kulinda maisha na mali ya wananchi. Ninakemea vitendo ambavyo vinafanywa na hawa wahalifu. Inapaswa Serikali iwachukue hawa kama magaidi kwa sababu sisi kama Wabunge tayari tumejitolea kupitisha Miswada. Inapaswa Serikali inunue vifaa dhabiti vya kupambana na hawa magaidi na wakora wakitumia hela ambazo inatoza ushuru. Naunga mkono. Asante."
}