GET /api/v0.1/hansard/entries/1385436/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1385436,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1385436/?format=api",
    "text_counter": 516,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "[Technical Hitch] --- kila Kaunti ya Kenya, hata Kaunti yetu ya Tana River. Bw. Spika wa Muda, hizi nafasi za kazi zinachangia kupunguza ukosefu wa nafasi za kazi hapa Kenya. Serikali inasema ya kwamba upungufu wa kazi kwa vijana wetu waliomaliza shule saa hii ni milioni tano. Tunataka kutoa nafasi za kazi kwa vijana wetu. Kwa hivyo, tukianza programme hii, vijana wetu wengi watapata kazi. Nimefurahia sana nilipoona ripoti ya Chairman wa Kamati inayohusika na Ardhi na Ujenzi wa Nyumba, akisema ya kwamba sheria hii tunayotengeneza inaunda boardk atika kila kaunti. Hizi board zitasaidia kuleta mawazo tofauti wakati ambao tunaenda kutumia hela ambazo tutazichukua kupitia hii sheria. Bw. Spika wa Muda, kwa mfano, kule Tana River, hatungependa kujengewa sky scrapers, ama nyumba ambazo zinaenda juu. Tuko na nafasi kubwa, tunataka tujengewe nyumba zile tumezoea. Wengine wetu tukipandishwa majumba ya juu, tunakuwa na wasiwasi kwamba hizi nyumba zinaweza kuanguka. Tumeona kwa runinga mambo haya yakifanyika. Kule kwetu, tuko na nafasi kubwa na tungependa wakati ambao hizi nyumba zitajengwa, ziwe zinajengwa kuhusiana na matakwa ya wananchi wa sehemu hiyo."
}